AINA ZA SHULE
CALENDA YA SHULE
WALIMU NA WAFANYAKAZI
Kujua Kiingerza
KUSAJILI SHULENI
JUA HAKI NA WAJIBU WAKO
RUHUSA YA LUGHA
KUHUDURIA
MAHITAJI YA CHANJO
KUUNGA MTOTO WAKO MKONO NYUMBANI
RASILIMALI ZAIDI
Aina za shule
Kuna aina za shule za umri tofauti:
Kalenda ya shule
Wajibu wa mwalimu / Wafanyikazi
Waelekezi
Waelekezi hawafunzi wanafunzi. Wamesimamia Shule. Kuna aina tofauti ya waelekezi:
Mwelekezi mkuu: Mwelekezi mkuu anasimamia wilaya nzima ya shule.
Mwalimu Mkuu: Kila shule kwa wilaya ina mwalimu mkuu ambaye anasimamia shule. Mwalimu mkuu huwasiliana na walimu, wanafunzi, na familia za wanafunzi.
Msaidizi Mkuu: Kila shule ina moja au zaidi wakuu msaidizi anayewasaidia shule kuu.
Walim
Walimu hufunza wanafunzi darasani. Kuna aina tofauti za walimu:
Walimu wa daras: Chekechea hadi gredi la 5, wanafunzi huwa wanashinda na mwalimu wao wa darasa siku nyingi za shule. Mwalimu wao wa darasa wakati mwingi hufunza masomo mengi ya shule, kama vile kusoma, hesabati, masomo ya jamii, na sayansi.
Walimu Wataalamu: katika shule ya kati (gredi 6-8) na shule ya upili (gredi 9-12), wanafunzi wana walimu tofauti ambao wamefuzu kwa sehemu Fulani ya utaalamu, kama vile Sanaa za lugha ya Kiingereza, hesabati, sayansi, masomo ya jamii, masomo ya jamii ya mwili, sanaa, na kadhalika….
Walimu wa kukuza Lugha (ELD): Walimu wa ELD wanashirikiana na walimu wa darasa na ujuzi kukuza uwezo katika lugha ya Kiingereza wa kusikiliza, kuzungumza, kusoma, na kuandika, na pia ufahamu wa kitamaduni.
Mwalimu wa Elimu spesheli: Walimu wa elimu spesheli wanawaunga mikono wanafunzi ambao wanamahitaji tofauti ya kimasomo, kihisia, na / au ya kimwili.
Wafanyikazi wa shule
Kando na walimu, kuna wafanyikazi wengine ambao wanasaidia wanafunzi na familia, kama vile:
Mshauri wa shule: Washauri wa shule wanashauri wanafunzi kwa elimu yao, kuwasaidia kuchagua madarasa na kubuni ratiba, na pia kuwasaidia na mahitaji yao ya kijamii, kihisia, na ya kitabia. Wanaweza kukusaidia kupata ujumbe kuhusu shule na misaada na rasilimali ya jamii.
Muuguzi wa shule: Muuguzi wa shule anasaidia wanafunzi ambao ni wagonjwa au wameumia.
Mtaalamu wa rasilimali za shule na familia (SFRS): Mtaalamu wa rasilimali za shule na familia wanawasaidia wanafunzi na familia ambazo wana mahitaji mbali mbali za kijamii, kitabia, na ya kimwili. Wanaweza saidia kwa mawasiliano ya nyumbani / shule kwa kutembelea nyumba na kuungananisha familia kwa huduma za shule na jamii.
Afisa wa Rasilimali za Shule (SRO): SRO ni afisa wa polisi waliohitimu amabao wanasaidia wanafunzi na wafanyikazi kuwa salama katika nyanja za shule.
Karani: Karani wa shule anafanya kazi kwa afisi kuu, na anaweza saidia kuunganisha familia na waelekezi na walimu. Wanaweza pia kuweka rekodi kama mtoto wako ako shuleni au ametohudhuria. Unafaa kuwasiliana na karani wa shule au afisi ya kuhudhuria kama mtoto wako hatakuwa shuleni.
Haki za wazazi na wajibu
Kama mzazi alio na mtoto kwa mfumo wa shule wa Marekani, ukona haki na wajibu. Jedwali hili linafupisha zote:
UnaHAKI sì:
- Kujua jinsi mtoto wako anaendelea shuleni
- Kukutana na walimu kuhusu kazi ya shule ya mtoto wako na hatua za kiakademia
- Kujua ni nini mtoto wako ansoma shuleni
- Kuomba shule msaada kama mtoto wako anawakati mgumu kuona, kusikia, au kusoma shuleni
- Kujua maana za karatasi za shule kabla ya kuzitia sahihi
- Kujua ni programu zipo zenye zinaweza sayia mtoto wako
- Kujua mtoto wako akiwa mashakani na jinsi shule itakavyofanya
- Kuenda mikutano ya shule
- Kupokea misaada ya utafsiri wa lugha unapokutana na walimu au wafanyikazi wa shule.
UnaWAJIBU wa:
- Kuhakikisha mtoto wako anaenda shuleni kwa wakati, kila siku, pengine kama ni mgonjwa.
- Kuhakikisha mtoto wako anafany kazi yake ya ziada kila siku
- Kuhakikisha mtoto wako ni safi; amelishwa; anavalia nuo safi, na analala vizuri.
- Kuhakikisha mtoto wako anaelewa jinsi ya kujibeba shuleni na anafuata sheria zilizobuniwa na mwalimu. Sheria hizi zinaweza kuwa:
- Lazima watoto wasikilize mwalimu na kufanya vile mwalimu anawaambia.
- Wanaiunua mikono yao ili wazungumze.
- Wanasimama kwa foleni na kutembea pamoja shuleni.
- Hawagongi au kupigana.
- Motore Hawatishi Watoto.
- Hawatumii maneno mabaya.
- Wanafanya kazi pamoja na wanafunzi wengine.
- Wanakuja kwa wakati darsani.
- Wanamaliza kazi yao ya ziada na kuileta hadi shuleni.
Kuunga mtoto wako mkono nyumbani
Unaweza kuwa unawaza jinsi, kama mzazi, vile unaweza kusaidia kuunga mkono hatua za kilingua na kiakedemia da mtoto wako. Ndio hizi namna kadha:
- Kuwa na subira. Elewa kuwa kujua lugha ni njia ngumu, na ni ndefu.
- Kujua lugha mpya inachukua nguvu nyingi sana. Hakikisha mtoto wako anapata mapumziko ya kutosha.
- Tayarisha mahala palipotulia na wakati wa kawaida wa kufanya kazi ya ziada au kusoma.
- Zungumza na mtoto wako kuhusu chenye kinafanyika shuleni.
- Wasiliana na mwalimu wa mtoto wako na ushiriki kwa mikongamano ya mzazi-mwalimu.
- Himiza mtoto wako kukuonyesha kazi zote za shule.
- Tunza lugha yako ya kaisili. Kuwa mbilingua ni uwezo mzuri sana!
- Kusoma na mtoto wako kwa usomi na uandishi wowote kwa lugha ya kiasili utahamisha na kuunga mkono kukuza kwa usomi na uandishi kwa lugha ya Kiingereza.
RASSILIMALI YA FAMILIA NA JAMII
-
Kituo cha wakimbizi
-
Shule za jamii
-
Elimu ya watu wazima / jopo la usomi na uandishi
-
Zahanati za Afya