Together we can
Kiswahili

Elimu katika Shule ya Wilaya ya Lancaster

Shule ya Wilaya ya Lancaster ni shule ya umma. Kila mtoto ana haki ya kuenda shule ya umma bila gharama yoyote. Je, nini inahitajika kusajili mtoto katika Shule ya Wilaya ya Lancaster? Ni kina nani huwa unawaona shuleni? Unazungumza na nani kama unatatizo au mtoto wako anashida? Ni umri gani watoto huanza shule, na siku shuleni ni wa muda upi? Jinsi ya kufanya kama ni lazima mtoto wako atohudhurie darasa? Tuna majibu na rasilimali ya kukusaidia kujiunga na shule Marekani.

AINA ZA SHULE

KALENDA YA SHULE

WALIMU NA WAFANYAKAZI

KUJUA KIINGERZA

KUSAJILI SHULENI

JUA HAKI NA WAJIBU WAKO

RUHUSA YA LUGHA

KUHUDHURIA

MAHITAJI YA CHANJO

KUUNGA MTOTO WAKO MKONO NYUMBANI

RASILIMALI ZAIDI

Aina za shule

Kuna aina za shule za umri tofauti:

Kalenda ya shule

Kalenda ya shule Marekani huanza mwisho wa Agosti na huisha Juni mapema.  Katika mwaka wa shule, watoto wanahudhuria shule Jumatatu hadi Ijumaa.  Watoto hawaendi shuleni siku ya Jumamosi na Jumapili.

Wajibu wa mwalimu/Wafanyikazi

Waelekezi

Waelekezi hawafunzi wanafunzi. Wamesimamia shule. Kuna aina tofauti ya waelekezi:

Mwelekezi mkuu:  Mwelekezi mkuu anasimamia wilaya nzima ya shule.

Mwalimu mkuu: Kila shule kwa wilaya ina mwalimu mkuu ambaye anasimamia shule. Mwalimu mkuu huwasiliana na walimu, wanafunzi, na familia za wanafunzi.

Msaidizi Mkuu:   Kila shule ina moja au zaidi wakuu msaidizi anayewasaidia shule kuu.

walimu

Walimu hufunza wanafunzi darasani. Kuna aina tofauti za walimu:

Walimu wa darasa: Chekechea hadi gredi la 5, wanafunzi huwa wanashinda na mwalimu wao wa darasa siku nyingi za shule. Mwalimu wao wa darasa wakati mwingi hufunza masomo mengi ya shule, kama vile kusoma, hesabati, masomo ya jamii, na sayansi.

Walimu wataalamu: katika shule ya kati (gredi 6-8) na shule ya upili (gredi 9-12), wanafunzi wana walimu tofauti ambao wamefuzu kwa sehemu Fulani ya utaalamu, kama vile Sanaa za lugha ya Kiingereza, hesabati, sayansi, masomo ya jamii, masomo ya mwili, sanaa, na kadhalika….

Walimu wa kukuza Lugha (ELD):  Walimu wa ELD wanashirikiana na walimu wa darasa na ujuzi kukuza  uwezo katika lugha ya Kiingereza wa kusikiliza, kuzungumza, kusoma, na kuandika, na pia ufahamu wa kitamaduni.

Mwalimu wa Elimu spesheli: Walimu wa elimu spesheli wanawaunga mikono wanafunzi ambao wanamahitaji tofauti ya kimasomo, kihisia, na/au ya kimwili.

Wafanyikazi wa shule

Kando na walimu, kuna wafanyikazi wengine ambao wanasaidia wanafunzi na familia, kama vile:

Mshauri wa shule: Washauri wa shule wanashauri wanafunzi kwa elimu yao, kuwasaidia kuchagua madarasa na kubuni ratiba, na pia kuwasaidia na mahitaji yao ya kijamii, kihisia, na ya kitabia.  Wanaweza kukusaidia kupata ujumbe kuhusu shule na misaada na rasilimali ya jamii.

Muuguzi wa shule:  Muuguzi wa shule anasaidia wanafunzi ambao ni wagonjwa au wameumia.

Mtaalamu wa rasilimali za shule na familia (SFRS):  Mtaalamu wa rasilimali za shule na familia wanawasaidia wanafunzi na familia ambazo wana mahitaji mbali mbali za kijamii, kitabia, na ya kimwili. Wanaweza saidia kwa mawasiliano ya nyumbani/shule kwa kutembelea nyumba na kuungananisha familia kwa huduma za shule na jamii.

Afisa wa Rasilimali za Shule (SRO):  SRO ni afisa wa polisi waliohitimu amabao wanasaidia wanafunzi na wafanyikazi kuwa salama katika nyanja za shule.

Karani: Karani wa shule anafanya kazi kwa afisi kuu, na anaweza saidia kuunganisha familia na waelekezi na walimu.  Wanaweza pia kuweka rekodi kama mtoto wako ako shuleni au ametohudhuria. Unafaa kuwasiliana na karani wa shule au afisi ya kuhudhuria kama mtoto wako hatakuwa shuleni.

Haki za wazazi na wajibu

Kama mzazi alio na mtoto kwa mfumo wa shule wa Marekani, ukona haki na wajibu. Jedwali hili linafupisha zote:

UnaHAKI ya:

  • Kujua jinsi mtoto wako anaendelea shuleni
  • Kukutana na walimu kuhusu kazi ya shule ya mtoto wako na hatua za kiakademia
  • Kujua ni nini mtoto wako ansoma shuleni
  • Kuomba shule msaada kama mtoto wako anawakati mgumu kuona, kusikia, au kusoma shuleni
  • Kujua maana za karatasi za shule kabla ya kuzitia sahihi
  • Kujua ni programu zipo zenye zinaweza saidia mtoto wako
  • Kujua mtoto wako akiwa mashakani na jinsi shule itakavyofanya
  • Kuenda mikutano ya shule
  • Kupokea misaada ya utafsiri wa lugha unapokutana na walimu au wafanyikazi wa shule.

UnaWAJIBU wa:

  • Kuhakikisha mtoto wako anaenda shuleni kwa wakati, kila siku, pengine kama ni mgonjwa.
  • Kuhakikisha mtoto wako anafanya kazi yake ya ziada kila siku
  • Kuhakikisha mtoto wako ni safi; amelishwa; anavalia nguo safi, na analala vizuri.
  • Kuhakikisha mtoto wako anaelewa jinsi ya kujibeba shuleni na anafuata sheria zilizobuniwa na mwalimu. Sheria hizi zinaweza kuwa:
    • Lazima watoto wasikilize mwalimu na kufanya vile mwalimu anawaambia.
    • Wanaiunua mikono yao ili wazungumze.
    • Wanasimama kwa foleni na kutembea pamoja shuleni.
    • Hawagongi au kupigana.
    • Hawatishi watoto wengine.
    • Hawatumii maneno mabaya.
    • Wanafanya kazi pamoja na wanafunzi wengine.
    • Wanakuja kwa wakati darsani.
    • Wanamaliza kazi yao ya ziada na kuileta hadi shuleni.

Kuunga mtoto wako mkono nyumbani

Unaweza kuwa unawaza jinsi, kama mzazi, vile unaweza kusaidia kuunga mkono hatua za kilingua na kiakedemia za mtoto wako. Ndio hizi namna kadha:

  • Kuwa na subira. Elewa kuwa kujua lugha ni njia ngumu, na ni ndefu.
  • Kujua lugha mpya inachukua nguvu nyingi sana. Hakikisha mtoto wako anapata mapumziko ya kutosha.
  • Tayarisha mahala palipotulia na wakati wa kawaida wa kufanya kazi ya ziada au kusoma.
  • Zungumza na mtoto wako kuhusu chenye kinafanyika shuleni.
  • Wasiliana na mwalimu wa mtoto wako na ushiriki kwa mikongamano ya mzazi-mwalimu.
  • Himiza mtoto wako kukuonyesha kazi zote za shule.
  • Tunza lugha yako ya kaisili. Kuwa mbilingua ni uwezo mzuri sana!
  • Kusoma na mtoto wako kwa usomi na uandishi wowote kwa lugha ya kiasili utahamisha na kuunga mkono kukuza kwa usomi na uandishi kwa lugha ya Kiingereza.

RASILIMALI YA FAMILIA NA JAMII